4 Mei 2020 - 09:35
Rais Rouhani: Kuenea corona kumeziweka chini ya alama ya kuuliza siasa za kimataifa

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuenea kirusi cha corona kumeziweka chini ya alama ya kuuliza siasa za kimataifa na kusisitiza kuwa, leo hii walimwengu wanasema bila ya kificho kuwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran si vya kibinadamu na wanavilaani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo katika kikao cha Kamati ya Taifa ya Kusimamia na Kudhibiti Ugonjwa wa Corona humu nchini na huku akigusia jinsi corona ilivyoleta mabadiliko duniani amesema, katika dunia ambayo walikuwa wakidai kuwa njia pekee ya maisha ni kuwa na miungano mikubwa ya kieneo na kimataifa, baada ya kutokea corona; yote hayo yamesahaulika na badala yake nchi hazikusaidiana ipasavyo, bali zimekimbilia kwenye fikra zao za kitaifa na kudhoofisha miungano yao.

Huko Marekani kunafanyika ubaguzi katika matibabu, weusi wanabaguliwa na weupe na wenye asili ya Marekani wanabaguliwa na wasio na asili na nchi hiyo. Amesema, hata katika Umoja wa Ulaya pia nchi ambazo zilikuwa zikijifanya ni marafiki zinapapurana hata katika kumiliki vibarakoa.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia pia mafanikio yaliyopatikana ya kufanyiwa uchunguzi wa corona watu milioni 78 nchini Iran katika hatua ya awali ya mpango wa taifa zima wa kupambana na COVID-19 na kuongeza kuwa, katika awamu ya pili pia watu milioni 30 wameshashirikishwa kwenye zoezi hilo  na kwamba awamu hii ya pili inafanyika kwa kina zaidi na kwa ufanisi mkubwa zaidi. 

Aidha amewashukuru wananchi kwa kufuata maelekezo ya maafisa wa afya kiasi kwamba kiujumla asilimia 83 ya watu wamefuata maelekezo hayo huku baadhi ya miji ni asilimia 92 ya walioheshimu maagizo hayo. 

Vile vile amesema, katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, watu waliokwenda mahospitalini kwa ugonjwa wa corona wamepungua sana nchini Iran na wamekaribia watu 300.

342/